
Taifa limepoteza kiongozi jasiri, mzalendo – Dk. Mwinyi NA MWANDISHI WETU MAKAMU wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, amefariki dunia. Akitangaza kifo cha mwanasiasa huyo aliezaliwa Oktoba 22, 1943, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, alieleza kuwa Maalim Seif amefariki dunia jana katika hospitali ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu. “Majira ya saa 5:26 asubuhi, makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad. Maalim amefariki wakati akiendelea na matibabu katika hospitali ya muhimbili alipokuwa amelazwa tokea tarehe 9 mwezi huu,” alieleza Dk. Mwinyi katika taarifa yake kupitia televisheni ya Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC). Aidha Dk. Mwinyi alitoa pole kwa familia ya marehemu, viongozi na wanachama wa chama cha ACT Wazalendo, wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla akiwataka kuendelea kuwa watulivu na wavumilivu. Maalim seif ambae hadi mauuti yanamkuta alikuwa mwenyekiti wa chama cha...