Programu kuratibu maudhui ya filamu kuanzishwa
.jpeg)
NA SAIDA ISSA, DODOMA Na Saida Issa, Dodoma SERIKALI kupitia kamati ya kutetea haki za wasanii inatarajia kuanzisha programu ya kuratibu uandaaji wa filamu zenye maudhui ya kutangaza utajiri wa nchi katika eneo la utamaduni, historia na jiografia yake. Hayo yalibainishwa jijini hapa jana, na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) Dk. Kiagho Kilonzo (pichani) wakati akizungumza na wandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa shughuli za bodi na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti ya mwaka huu wa fedha. Amesema hadi sasa Kamati ya kutetea Haki za Wasanii imeshapokea malalamiko 30 na kuyashughulikia, huku takribani sh. milioni 300 zilizokuwa zimedhulumiwa zimesharejeshwa kwa wasanii. Alisema lengo la filamu hiyo ni kujenga mapenzi hasa kwa vijana wa kitanzania kwa nchi yao kwa kuwaongezea ufahamu wa rasilimali waliyonayo. “Programu hii itasaidia kutunza kumbukumbu za kihistoria kwa kuhusisha taarifa za viongozi wetu mbalimbali waliofanya mambo makubwa kama vile Mwl....