
Majaliwa awawashia moto watendaji wanaodaiwa 'kukwapua' mamilioni NA MWANDISHI WETU, DODOMA WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa (pichani) amewasimamisha kazi mkaguzi Mkuu, Mkaguzi Msaidizi na baadhi ya watendaji wa wizara ya Fedha na Mipango ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za umma zinazowakabili. Alichukua hatua hiyo katika kikao kazi na waziri wa Fedha na Mipango, Kaibu Mkuu, Manaibu Katibu Wakuu na Watendaji Waandamizi wa Wizara hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma. Mbali ya hatua hiyo, Majaliwa amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Kamishna wa Polisi, CP Salum Rashid Hamdun kufanya uchunguzi kuhusu tuhuma hizo na ikithibitika kwamba tuhuma si za kweli wahusika watarejeshwa kazini. Majaliwa alizitaja baadhi ya tuhuma hizo kuwa ni malipo yaliyofanyika Machi 31, mwaka huu kupitia vocha 30 ya shilingi milioni 251 yakielezwa kuwa ni malipo m...